Serikali imepokea msaada wa Faranga za Uswisi milioni 15.75 sawa na shilingi Bilioni 39.59 kwa ajili ya kugharamia mradi wa uboreshaji wa afya na uimarishaji wa mfumo wa afya pamoja na kugharamia program ya kutokomeza Malaria nchini.
Akipokea msaada huo Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James amesema lengo kuu la msaada huo ni uanzishwaji wa huduma ya msaada wa kitaalam kwa Serikali chini ya utaratibu wa kituo cha kuimarisha mifumo ya afya kilichopo Ofisi ya Rais TAMISEMI.
Aidha, James amesema msaada huo utatumika kuwezesha mpango wa kudhibiti Malaria Tanzania ili kuondoa kabisa vifo vinavyotokana na malaria na kupanua wigo wa maeneo yasiyokuwa na malaria (Malaria Free Zones).
James amesema kuwa hii ni mara ya pili katika kipindi cha siku 30 zilizopita kwa Serikali ya Uswisi kuipatia Tanzania msaada wa kuboresha masuala ya afya ambapo tarehe 6 Oktoba, 2020 nchi hiyo iliipatia Tanzania shilingi bilioni 44.10 na kufikisha kiwango cha msaada katika kipindi hicho kufikia sh. Bilioni 83.7
‘Nchi zetu mbili zina uhusiano mzuri unaoendelea kukua kama unavyothibitishwa na kuongezeka kwa idadi ya miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Serikali za Uswisi’ James