Mkuu wa Oparasheni na Mafunzo wa Jeshi la Wananchi JWTZ Meja Jenerali Alfred Kapinga ameshangazwa na umahiri wa Askari wa kike waliolipua bomu la kivita RPG-7 kwa mara ya kwanza wakati wa kufunga mafunzo makubwa kundi la 23 ya mwaka 2020 katika kituo cha Mafunzo ya Kijeshi Kalunde Tabora.
Meja Jenerali Kapinga amesema “Mpaka nazeeka sasa nilikuwa sijaona wanadada wanapiga RPG sisi tushazoea kazi hii niya kina baba lakin leo nimeshuhudia askari wa kike wanapiga RPG-7V”.