Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, John Magufuli amefichua siri jinsi alivyomfahamu aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na Mbunge wa Jimbo la Karatu Balozi Dkt. Willibroad Slaa kwa jinsi alivyokuwa tofauti na wapinzani wengine.
Balozi Dkt. Slaa alihama CHADEMA wakati vuguvugu la Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, baada ya kutoridhishwa na uamuzi wa Chama hicho kikiungana na Vyama vilivyokuwa vikiunda UKAWA kumpitisha Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa kuwa Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano .
Akizungumza Jimboni Karatu mkoani Arusha kwa ajili ya kuomba kura kwa wananchi, Magufuli amesema Balozi Dkt. Slaa alikuwa ni tofauti na wapinzani wengi kwa jinsi alivyokuwa mtu makini,mwenye kujenga hoja na alikuwa mwakilishi mzuri wa wananchi wa jimboni kwake.
“Wakati alipotaka kuja kuomba ubunge huku (karatu)aliomba nafasi hiyo kupitia Chama cha Mapinduzi kwasababu yeye alikuwa mwanaccm,Chama cha mapinduzi hapa karatu wakamfanyizia figisu hawakulirudisha jina lake ndipo akaamua kwenda mageuzi,” JPM
“Balozi Dkt.Slaa baada ya kukaa upinzani na kuona ubabaishaji kwenye Chama hicho aliamua kujitoa katika Chama hicho,” JPM