Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba, amesema atakapopata ridhaa ya kuwaongoza Watanzania, Serikali yake itashirikiana na Jumuiya ya Umoja wa Kimataifa ili kuweza kuwekeza katika mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Profesa Lipumba ameyasema hayo wakati akihutubia wananchi wa Kijiji cha Kipindimbi, Kata ya Njinjo, jimbo la Kilwa Kaskazini ambapo amesema serikali ya CUF kwa kushirikiana na wananchi itahakikisha wananchi wanaondokana na maafa ya mafuriko.
”Pana tatizo ambalo linaweza kuwa la muda mrefu tatizo la mabadiliko ya tabia nchi ni tatizo ambalo tayari limeshatufikia, nchi zilizoendelea zimekuwa zikizalisha hii hewa ukaa ambayo imeongeza joto Duniani” Prof. Lipumba
“Tunahitaji tuwe na serikali itakayoshirikiana na wananchi na Jumuiya ya Kimataifa ili kuweza kukabiliana na tatizo hilo la mabadiliko ya tabia nchi” Prof. Lipumba.