Mgombea Urais kupitia chama cha Democratic nchini Marekani, Joe Biden, ameonekana kuongoza kwa point 10 dhidi ya Rais wa sasa, Donald Trump.
Hojaji iliyofanywa na Shirika la Habari la NBC na Gazeti la Wall Street imeonyesha idadi ya wapiga kura wanaomuunga mkono Joe Biden imefikia asilimia 52 dhidi ya asilimia 42 ya Trump.
Hojaji hiyo ya mwisho imefanyika Oktoba 29 hadi 31, pia imeonyesha Joe Biden ana nafasi kubwa zaidi kwa Wamarekani wenye asili ya Afrika, Vijana, Wazee na Wanawake.