Mgombea wa Urais kwa tiketi ya chama cha Democratic, Joe Biden anazidi kuashiria ushindi wake katika majimbo muhimi, wakati kwa upande wa mpinzani wake Donald Trump akiendelea kulalamikia kuchezewa rafu, na kushinikiza kisheria maeneo tata kusimamisha zoezi la kuhesabu kura.
Mpaka wakati huu Biden anahitaji nukta sita za wajumbe wa majimbo ilikufikia 270 inayohitajika kumuingiza Ikulu.
Biden anaongoza katika majimbo muhimu ya Pennyslavania Nevada and Georgia. Katika jimbo la Arizona kwa mfano ambako asilimia 94 za kura zimehesabiwa Biden ana asalimia 49.9 na Trump asilimia 48.6.
Pennsylavania ambako wapo katika asilimia 96 Trump ana asilimia 49.2 na Biden 49.5. Georgia ambako kumehisabiwa kwa asilimia 99% Biden ana asilimia 49.5 na Trump, 49.4 North Carolina kushahesabiwa asilimia 98% na Trump kapata asilimia 50.0 Biden ikiwa 48.6, Nevada asilimia 93% , Trump kapata 48.0 na Biden 49.8.