Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameahidi kuwatumikia watanzania bila kujali itikadi za vyama wala dini ili kuendelea kukuza uchumi wa taifa katika kipindi cha miaka mitano ya awamu ya pili ya uongozi wake.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo baada ya kushiriki ibaada katika Parokia ya Bikra Maria Imakulata iliyopo Chamwino Ikulu jijini Dodoma, ambapo amewataka Watanzania kuwa kitu kimoja baada ya kumalizika kwa shughuli za Uchaguzi Mkuu.
“Nina deni kubwa sana la kuwatumikia Watanzania, kwakuwa ushindi nilioupata haujatoka Chama cha Mapinduzi pekee bali ni kwa Watanzania wote walionichagua. Imani yao kwangu sitowaangusha nitapambana kukuza uchumi wa Tanzania yetu”JPM
Aidha amewahimiza watanzania kuendelea kufanya ibaada na kumtanguliza Mungu kwenye kila jambo, ili kudumisha amani, umoja na upendo kwa taifa.