Rais wa Iran Hassan Rouhani amemtolea wito Rais mteule wa Marekani Joe Biden kulirudisha tena taifa hilo katika makubaliano ya kinyuklia yaliyosainiwa mwaka 2015, kati ya Iran na mataifa yenye nguvu ya magharibi.
Rais Donald Trump aliiondoa Marekani kwenye makubaliano hayo mnamo mwaka 2018 na kuiwekea vikwazo vikali vya kiuchumi Tehran.
Mbali na Iran, mataifa kadhaa kote duniani yametuma salama za pongezi kwa Rais mteule Biden, wa chama cha Democratic kufuatiab uchindi wake wa uchaguzi wa Novemba 3.
Viongozi wengi ulimwenguni wameeleza matumaini yao kufanya kazi na Biden kwa umoja na ushirikiano, baada ya miaka minne ya sera za kibabe za Rais Trump.
Ingawa Trump amekataa kukubali matokeo ya uchaguzi, viongozi wengi ulimwenguni wameunga mkono tangazo la ushindi wa Biden na mgombea wake mwenza Kamala Harris.
VIA: DW Swahili