Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, amewataka watendaji ndani ya serikali kuchaopa kazi na kuachana na wasiwasi wa kuhisi atawaondoa.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo Novemba 9, 2020. kwenye hotuba yake baada ya kumwapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali Prof. Adelardus Kilungi Ikulu Chamwino, jijini Dodoma.
“Wakuu wa mikoa na wilaya msiwe na wasiwasi na inawezekana pasitokee mabadiliko yoyote labda kwa atakayestaafu au atakayefanya mambo ya hovyo, kama nilikuteua uwezo si bado ni ule ule najua wananisikia wachape kazi wasipochapa kazi shauri yao” Rais Magufuli
“RC unakuwa na wasiwasi gani labda kama ‘performance’ yako ilikuwa haifanyi kazi vizuri, nashangaa napata vimeseji kwamba Rais nimejitahidi katika kipindi changu, kana kwamba kipindi chake nilimwambia kinaisha baada ya mimi kuapishwa” Rais Magufuli