“Tunayofuraha tumekamilisha utaratibu wa michakato wa Wanafunzi waliomba mikopo kwa wale wenye vigezo, majina ya waliopangiwa mikopo sasa yapo tayari, kinachofuata kuanzia leo ni kupeleka pesa za malipo ya Wanafunzi kulingana na utaratibu wa Vyuo tofauti” Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru
“Tunayofuraha kuwatangazia kwamba baada ya kupokea taarifa za udahili kutoka TCU tumechakata, Wanafunzi wa mwaka wa kwanza wapatao 47305 hao ni wanafunzi wapya wamepangiwa mkopo, fedha waliyopangiwa hawa ni Bilioni 150” Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru