Kwa mujibu wa Ripoti ya The Washington Post, zaidi ya Maafisa wa Idara ya Usalama 130 nchini Marekani wamethibitishwa kupata COVID19 na kutakiwa kujitenga. Miongoni mwa majukumu ya Maafisa hao ni pamoja na kumlinda Rais Donald Trump.
Maambukizi yamehusishwa na mchakato wa Kampeni kabla ya Uchaguzi uliofanyika mapema mwezi huu ambapo Rais Trump, baadhi ya Wanafamilia wake wa karibu na Maafisa wa Ikulu waligundulika kuwa na Corona Virus.
Ripoti ya Maafisa hao inakuja wakati hali ya mlipuko inaendelea kuwa mbaya nchini humo. Visa vipya zaidi ya 153,000 viliripotiwa Alhamisi na jumla ya watu Milioni 10.6 wamekutwa na maambukizi hadi sasa.