Rais wa Uganda Yoweri Museveni atasimamia mazungumzo ya kuleta amani nchini Ethiopia kati ya Serikali na Maafisa wa eneo la Tigray.
Naibu Waziri Mkuu wa Ethiopia, Demeke Mekonnen Hassen, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje pamoja na Wawakilishi wa Tigray, wanatarajiwa kuwasili nchini Uganda leo (Jumatatu) ili kuanza mazungumzo hayo.
Kiongozi wa eneo la Tigray, amethibitisha Wapiganaji wake walifanya mashambulizi ya roketi kwenye Uwanja wa Ndege katika mji Mkuu wa Eritrea. Shambulizi hilo linaongeza wasiwasi wa vita katika eneo hilo la Pembe ya Afrika.