Imebainika kuwa watu wengi wanaishi na ugonjwa wa sukari bila kujijua, hivyo wataalamu wameshauri wananchi kujenga tabia ya kupima afya zao ili waweze kukabili ugonjwa huo.
Aidha, rekodi za Chama cha Wagonjwa wa Kisukari Tanzania (TDA), zinaonesha zaidi ya watoto 4,000 wanaishi na kisukari huku kikitaja ugonjwa huo kuwa ni tatizo kubwa kutokana na idadi ya watu kuongezeka.
Meneja wa TDA, Happy Nchimbi amesema ili kupata takwimu hizo, chama kimekuwa kikiangalia vituo au kliniki ambazo zipo kwenye hospitali za mikoa zilizoanzishwa kwa jitihada za chama kusaidia watoto baada ya kugundulika kwamba wao pia wanapata kisukari.
Via: Habarileo