Mchungaji maarufu barani Afrika, Bushiri ametoroka nchiniAfrika kusini baada ya kuachiwa kwa dhamana mapema mwezi huu kwa kushtakiwa kwa utapeli na utakatishaji fedha.
Mchungaji Bushiri, ambaye amesema kuwa anataka kusafisha jina lake, amerejea katika nchi yake, Malawi, akiwa na mke wake Mary na kusema kuwa kulikuwa na majaribio kadhaa ya kutishia maisha yake na mamlaka ya Afrika Kusini haikutoa ulinzi wowote kwake.
Kupitia mitandao ya kijamii mchungaji Bushiri amesema kukwepa dhamana ni njia ya busara ya kulinda maisha yake huku kukiwa kuna maswali ni namna gani mchungaji huyo ameweza kutoroka Afrika Kusini na kurudi kwao na kama mataifa hayo mawili yatashirikiana kumkamata na kumrejesha Afrika Kusini asikilize kesi yake.
Aidha yapo madai kuwa Bushiri alitoroka na ndege ya rais wa Malawi, Lazarus Chikwera, lakini ofisi ya Rais wa Malawi ulikanusha madai hayo lakini Waziri wa Mambo ya Nje nchini Malawi, Eisenhower Mkaka atahusishwa katika suala hilo.
Naye Waziri wa sheria wa Afrika Kusini, Ronald Lamola ameweka wazi kuwa serikali nchini humo haitasita kufuatilia suala hilo.
LIVE: JPM AMEMUAPISHA MAJALIWA KUWA WAZIRI MKUU, MPANGO PAMOJA NA KABUDI