Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli, amesema kuwa mbunge wa Jimbo la Isimani, William Lukuvi, pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje, Prof. Palamagamba Kabudi, hawawezi kuwa marais kwa sababu umri wao ni mkubwa.
“Wajumbe wa NEC walikuwa akina Lukuvi, tangu aingie mle ni mjumbe wa NEC, lakini urais hakuupata na sina uhakika kama ataupata, sasa ana miaka zaidi ya 60, yaani kwenye Kamati Kuu tuchague Rais anayenizidi umri mimi” JPM
“Maneno mengine yanaumiza lakini nataka niwaeleze mjitayarishe kisaikolojia kusudi msije mkapoteza hela zenu, hata wewe Prof. Kabudi hauwezi ukawa Rais, Kikwete wakati anaondoka alisema hataona Rais anayemzidi umri” Rais Magufuli