Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Pwani imewakatama Wahamiaji haramu zaidi ya 150 katika Wilaya ya Bagamoyo ambao walikuwa wakifichwa ili wasafirishwe kwenda Mikoa mingine kuelekea Afrika ya Kusini.
Hayo yameelezwa na Afisa uhamiaji Mkoa wa Pwani DCI Paul Eranga akiongea na waandishi wa habari Wilayani Bagamoyo.
“Tatizo la Uhamiaji katika Ukanda huu wa Bagamoyo ni kubwa ndani ya muda mfupi tumekamata zaidi ya wahamiaji haramu 155, tumekamata na Watanzania wenzetu 2 ambao wamewezesha hawa kuingia Tanzania” Afisa Uhamiaji Mkoa wa Pwani
“Hatutalala mpaka tuhakikishe hawa wanaowasaidia hawa Wahamiaji kuingiia nchini tunawakata wote na tunawafikisha katika vyombo vya sheria, walijaribu kutaka kutohonga fedha kiasi cha Milioni 7 na wakatangaliza 1.7m tuwaachie watu wao dili likifanikiwa watakuja kumalizia, tumewapata na tutawafikisha Mahakamani” Afisa Uhamiaji Mkoa wa Pwani