Kijana, Isaack Kawogo(24) aliyempora Askari magereza silaha aina ya SMG Usigani mkoani Iringa ameuawa kwa kupigwa risasi na Polisi baada ya kumjeruhi kaka yake, Andres Kawogo(61) akimtuhumu kuuza mashamba na kushindwa kumtoa gerezani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamis Issah amesema tukio hilo limetokea Novemba 20, huko maeneo ya Chaugingi mjini Njombe.
Amesema Kawongo aliiba silaha na kuitumia kufanya uhalifu ambapo alifanya matukio kadhaa Mkoani Iringa ikiwemo kumshambulia Askari kwa panga hali iliyosababisha wafungwa wengine kutoroka.
“Hii ni silaha ambayo askari magereza wanaitumia katika ulinzi wa wafungwa hao sasa huyu kwakuwa ni mhalifu akawa anaitumia katika kufanya uhalifu,” Kamanda Issah.
Amesema silaha hiyo ilikuwa na risasi kumi lakini mpaka inakamatwa na askari ilikuwa imebakiwa na risasi mbili pekee huku risasi nane zikitumika kufanya ualifu maeneo tofauti ikiwemo tukio hilo lilotokea Mkoani Njombe la kumjeruhi kaka yake.
Amesema licha ya juhudi kufanyika za kutaka kuokoa maisha yake ili alieleze Jeshi la Polisi namna alivyoondoka na silaha lakini ilishindikana kwa kuwa umauti ulimfika.
” Ukimnyang’a askari silaha namna pekee ya kuipa hiyo silaha ni kwa kutumia silaha hivyo wanapaswa kuwa makini,” Kamanda Issah