Waendesha mashtaka nchini Argentina wanamchunguza Daktari wa, Diego Maradona(60) kwa uwezekano wa kuua kufuatia kifo cha nyota huyo wa soka kilichotokea Novemba 26,2020.
Polisi Mjini Buenos Aires wameisaka nyumba na kliniki ya daktari huyo Leopoldo Luque huku wakijaribu kubaini iwapo ulikuwepo uzembe katika matibabu baada ya upasuaji aliofanyiwa Maradona.
Maradona alifariki dunia kutoka na shinikizo la damu nyumbani kwake ambako alikuwa akiendelea kupata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji.
Dokta Luque bado hajashtakiwa na amekuwa akikana kufanya kosa lolote.
Maradona alifanyiwa upasuaji kwenye mshipa wa ubongo kutokana na kuganda kwa damu, uliofanikiwa mapema mwezi huu na alikuwa akipata matibabu kutokana na uraibu wa pombe.