Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dkt. Edwin Mhede, amesema Serikali inapoteza zaidi ya Tsh. Bilioni 38 kwa mwaka kutokana na Mabasi kutotumia ukataji wa tiketi kwa njia ya mtandao (POS).
Aidha, Wamiliki wa Mabasi hupoteza zaidi ya Tsh. Bilioni 196 kila mwaka kwa kutotumia mfumo wa POS uliobuniwa maalumu kwa utoaji wa huduma ya usafiri.
Dkt. Mhede amesema ni vema kwa wasafirishaji kutumia mfumo huo ili kujitengezea faida na kukuza uchumi, kwa kuwa unalinda usalama wa chombo kwa kumfanya mmiliki kufuatilia mwenendo wa safari zake.
Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) kimesema wao hawana tatizo kutumia mfumo huo, wamehitaji wapewe elimu ya kutosha juu ya utumiaji wa mfumo.
“HUYU MTOENI ASIRUDI” MKURUGENZI ALIEMDHARAU WAZIRI MKUU ATUMBULIWA PAPO HAPO