Kenya imesema kwamba haijapokea ilani yoyote inayoitaka kumrudisha nyumbani balozi wake nchini Somalia kufuatia madai ya kuingilia masuala ya ndani na yale ya kisiasa ya taifa hilo.
Kenya pia ilipinga shutuma hizo ikizitaja kuwa zisizo na Ushahidi wowote.
Taarifa ya wizara ya Mambo ya Nje nchini Kenya imesema kwamba inaunga mkono kuimarika kwa Somalia na kuonya kwamba hatua hiyo huenda ikaathiri mchakato wa Mogadishu katika kujijenga upya.
”Serikali ya Kenya inaheshimu na kufuata sheria za kimataifa za uhuruwa kitaifa ,ule wa kieneo na pia kisiasa hususana kwa mataifa Afrika”.
Hatua hiyo ya Kenya inajiri baada ya Somalia siku ya Jumapili kumtaka balozi wake nchini Kenya Mohamud Ahmed Nur ‘Tarzan’ kurudi nyumbani kwa mazungumzo baada ya kuishutumu Kenya kwa kuingilia masuala yake ya nyumbani.
Somalia pia iliagiza balozi wa Kenya nchini Somalia Lucas Tumbo kurudi Nairobi.
Inadaiwa kwamba tangazo hilo lilitolewa baada ya bwana Nur Kuwasili nyumbani Somalia.
“HUYU MTOENI ASIRUDI” MKURUGENZI ALIEMDHARAU WAZIRI MKUU ATUMBULIWA PAPO HAPO