Bunge jipya la Kuwait litakuwa na Wanaume pekee kutokana na Wanawake wote waliogombea kushindwa kwenye uchaguzi wa Jumamosi ambapo kwenye Wagombea 326 kati yao kulikua na Wanawake 29 tu.
Wagombea wote kwa ujumla walikuwa ni Wagombea binafsi kwa kuwa Vyama vya siasa vimezuiwa nchini Kuwait, hii inakua mara ya kwanza tangu mwaka 2012 kwa bunge hilo kutokuwa na Mwanamke hata mmoja.
Mwanamke pekee aliyeingia katika Bunge lililopita alishinda katika uchaguzi wa marudio ambapo Mchambuzi wa siasa Mohammed al-Faili amesema Raia wa Kuwait wanataka sauti zenye nguvu bungeni ambazo wanawake hawana.