Rais Donald Trump wa Marekani ameiamuru Wizara ya Ulinzi wa Taifa na Makao Makuu ya Marekani barani Afrika AFRICOM kuondoa kikosi cha Marekani kutoka Somalia mwanzoni mwa mwaka kesho.
Idadi ya wanajeshi wa Marekani watakaorejeshwa kutoka Somalia bado haijajulikana, lakini wizara ya ulinzi ya Marekani inashauri kuondoa wanajeshi wote wa Marekani katika sehemu nyingine za Afrika.
Wizara hiyo imetoa taarifa ikisema, kutokana na amri hiyo, baadhi ya wanajeshi watapelekwa nje ya Afrika Mashariki, lakini kikosi cha Marekani nchini Somalia kitapelekwa katika nchi jirani ili kuendelea kuweka shinikizo dhidi ya magaidi nchini Somalia.
Habari zinasema, wanajeshi 700 wa Marekani nchini Somalia wanapambana na kundi la Al-Shabaab ambalo lina uhusiano na kundi la Al-Qaeda na kuanzisha mapigano ya kujaribu kupindua serikali ya Somalia.