Wananchi wa eneo la Ujiji Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma ambao wamebomolewa makaburi yao wameeleza kutoridhishwa na utaratibu unaotumiwa na Serikali katika ulipaji wa fidia ya makaburi hayo kwa ajili ya upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa mkoa huo.
Wakizungumza na AyoTV baadhi ya wananchi ambao makaburi yao yamevunjwa kwa ajili ya kupisha upanuzi wa uwanja wamesema utaratibu wa kila mtu kusimama juu ya kaburi ili kulipwa fidia haujatenda haki kulinga na mazingira ya eneo hilo.
Uamuzi wa Serikali na kuendelea na zoezi hili licha ya uwepo wa mgomo kwa baadhi ya wananchi ambapo nilizungumza na Meneja wa TANROAD Mkoa wa kigoma Mhandisi Narsisi Choma amesema zoezi hilol a kubomoa makaburi linaweza chukua siku mbili kisha taratibu nyingine kufuatwa.