Chama Kikuu cha Upinzani nchini humo, OFC kimetaka Viongozi wake kuachiwa huru kikisema itakuwa ngumu kujiandaa na Uchaguzi Mkuu bila wao.
OFC pia imetaka Ofisi zake zilizofungwa kufunguliwa na kuwepo uhuru wa kufanya kampeni nchi nzima kabla ya mchakato wa upigaji kura.
Viongozi wakuu wa Chama hicho walikamatwa July mwaka huu kufuatia vurugu zilizotokea baada ya kifo cha Mwanamuziki na Mwanaharakati maarufu, Hachalu Hundessa.
Uchaguzi Mkuu wa Ethiopia ulipangwa kufanyika Agosti lakini uliahirishwa hadi mwakani na tarehe rasmi bado haijatangazwa.