Mke wa Rais Mstaafu Kikwete ambaye pia ni Mbunge wa Mchinga, Lindi, Mama Salma Kikwete ameeleza jinsi alivyouanza uhusiano wake mpaka kuingia kwenye ndoa ili iwe mfano kwa Wasichana wa sasa.
Ni kwenye Kongamanono la Wasichana, Dar es salaam ambapo ametolea mfano wa maisha yake na jinsi alivyomsubirisha Mstaafu Kikwete enzi hizo hadi kumkumbalia ombi la kumuoa.
“JK Alikuja kufanya siasa Chuoni wakati huo akiwa katibu wa CCM Nachingwea akaniitaa ofisini kwake na kuniuliza umepata ujumbe wangu?” Mama Salma
“Alinitamkia ningependa nikuoe, akatoka akatununulia maembe na wezangu tukarudi Chuo, sikumjibu ndio au hapana mpaka nilipomaliza JKT, ndio maana alipoulizwa alisema yule Mwanamke amenisumbua kweli, msijirahisishe sio Mtu anakuambia ooh nakupenda, silali nakuwaza wewe… mkakubali kirahisi” – Mama Salma