Spika wa bunge la DRC, Jeanine Mabunda ameondolewa katika nafasi yake baada ya Wabunge kupiga kura ya maoni dhidi yake iliyowasilishwa bungeni na Upinzani.
Jana wabunge 281 kati ya 484 wa bunge hilo walisema kiongozi huyo aondoke kwenye nafasi hiyo .
Zaidi ya wabunge 200 kati ya 500 waalifanya kikao cha kupiga kura ya kumuondoa madarakani Spika wa bunge, Jeanine kutoka chama cha Joseph kabila.
Upande wa Chama cha Rais mstaafu Joseph Kabila tayari kulikuwa na mzozo katika vyama vilivyokuwa vinamuunga mkono, hivyo hiyo inaweza kuwa sababu ya kuanguka kwao.
Kwa sasa hatua inayofuata ni Waziri Mkuu kujiuzulu sasa kwa sababu Rais Felix Tshekedi atamchagua mtu atakayeunganisha vyama bungeni hivyo nia ya rais ni kuvunja muungano huo.
Hata hivyo swali linalowaumiza vichwa wengi inakuwaje spika huyo ashindwe kupata kura za kutosha kumtetea kupata kura za kutosha wakati wabunge wa chama chake ni wengi zaidi.