Katibu Tawala wa wilaya ya Bukoba, mkoani Kagera, Kadole Kilugala, amesema kuwa kama suala la mahari ni lazima katika jamii yetu basi iweze kutolewa kwa pande zote mbili yaani mwanamke apeleke zawadi upande wa mume na mume afanye vivyo hivyo ili kuweka usawa wa kijinsia.
Suala la mahari la upande mmoja ndiyo linaonekana kuwa ni linachochea masuala ya ukatili kwani wanaume huamua kuwafanyia chochote wanawake waliowaoa kwa kigezo cha wao kutoa mahari.
“Kama mahari ni lazima katika jamii yetu basi sote tuweze kutoa na kila mtu atoe kila alichonacho, mwanamke apeleke zawadi kwa mwanaume na mwanaume apeleke zawadi kwa mwanamke, tungeweza kutengeneza usawa kwa sababu mahari inatufanya tukose usawa wa kijinsia”,
DAS Kilugala.