Serikali ya Somalia imetangaza kusitisha uhusiano wake na Kenya ikidai kwamba Serikali ya Kenya inaingilia kati masuala yake ya ndani.
Nchi hiyo jirani wa Kenya, imetangaza kuwafukuza wanadiplomasia wote wa Kenya na kuagiza wanadiplomasia wake wote walio Nairobi kurudi Mogadishu ndani ya siku saba kuanzia leo Jumanne Desemba 15, 2020.
Waziri wa Habari wa Somalia, Osman Abukar Dubbe, amesema katika hotuba iliyorushwa moja kwa moja na televisheni ya serikali ya Somalia jana Jumatatu jioni kwamba hatua hiyo imechukuliwa kujibu uchokozi wa kisiasa wa kila mara unaofanywa na serikali ya Kenya kinyume na uhuru wa Somalia.
Hata hivyo Serikali ya Kenya haijajibu madai wala hatua hiyo ya Somalia.
Somalia ilimuondoa Balozi wake nchini Kenya Novemba 29 na kuamuru balozi wa Kenya kuondoka Mogadishu.
Wakati huo, Somalia iliishutumu Kenya kwa kuingilia kati maswala yake ya ndani na siasa za nchi hiyo