Captain wa Aston Villa Jack Grealish amefungiwa miezi tisa kuendesha gari na faini ya pound 82,499 (zaidi ya Tsh Milioni 248.2) kwa kukutwa na hatia ya kosa udereva mbovu (careless driver)
Hukumu yake imetolewa kwenye Mahakama ya Birmingham leo ambapo alikua na makosa mbalimbali ikiwemo kuyagonga na Range Rover yake magari mawili yaliyokua yameegeshwa na ushahidi umeonesha alikua amekunywa pombe.
Kosa jingine ni gari lake kunaswa likiwa spidi sana October 18 ambapo alinaswa bila kujua na Polisi aliyekua na gari la Polisi lisilo na nembo au utambulisho wa Polisi.
Faini hii ya zaidi ya Tsh. milioni 248 ikiwemo malipo ya uharibifu inatakiwa kulipwa ndani ya siku 7, na atatakiwa kuomba upya leseni ya Udereva kifungo chake kikiisha.