Waziri wa madini Dotto Biteko ametoa maagizo ya kuwafutia leseni ya uchimbaji wa madini wamiliki wa migodi ambayo wachimbaji wake atakamatwa akitorosha madini huku akiwataka mameneja wa migodi kuwakagua wafanyakazi kabla yakutoka kwenye ukuta wa Mirerani.
Biteko ametoa maagizo hayo leo Mirerani wilayani Manyara wakati akizungumza na wachimbaji na wafanyabiashara wa madini.