Shirika la afya duniani (WHO) limesema linafanya mawasiliano ya karibu na nchi ya Uingereza, kuhusiana na aina mpya ya virusi vya corona ambavyo vimeonesha usugu.
Taarifa kutoka Uingereza zinasema kuwa aina mpya ya virusi, vinaenea kwa kasi zaidi kuliko vile vya awali, lakini hawaamini ikiwa ni hatari.
Tayari maeneo mengi ya miji ya Kusini na Mashariki mwa Uingereza, kumetangazwa marufuku zaidi ya watu kutembea ili kudhibiti kuenea kwa maambukizi.
Hadi sasa hakuna ushahidi kuwa virusi hivi vilivyogunduliwa vinaonesha utofauti na chanjo ambayo inatolewa.