Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Katavi, inafanya uchunguzi wa wauguzi watatu wa Kituo Cha Afya Ilembo kilichopo Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, kwa tuhuma za wizi wa dawa za Serikali na kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa wagonjwa waliokuwa wamelazwa kwenye kituo hicho.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Katavi, Christopher Nakua amesema Hussein Hassan ni mmoja wa wauguzi hao, ambaye alikamatwa na begi likiwa na dawa za binadamu, ambazo ilibainika alikuwa akiwauzia wagonjwa kwenye wodi ya wazazi hasa nyakati za usiku.
“Hussein muuguzi kwenye wodi ya wazazi alikamatwa Desemba 14,2020, baada ya kuanza kuhojiwa na uongozi wa kituo hicho na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda alikiri kutenda kosa hilo lakini alikimbia kwa lengo la kujaribu kutoroka na aliacha pikipiki yake,” Nakua.
Pia muuguzi mwingine Charles Daniel aliye kwenye wodi ya wazazi katika kituo hicho, alibainika kuomba rushwa ya shilinigi 20,000 kwa mume wa mgonjwa aliyekuwa amelazwa katika kituo hicho, lakini alipewa shilingi 10,00 na mume wa mgonjwa uyo ili amsaidie mgonjwa wake kujifungua salama.