Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imewakabidhi zaidi ya Tsh. Milioni 88.8 raia waliotapeliwa na Kampuni za Mikopo zinazoendesha shughuli kinyume na utaratibu.
Urejeshaji wa fedha hizo umefanyika mbele ya Madiwani ili kuhamasisha ushirikiano na utendaji wa pamoja katika kupiga vita Vitendo vyote vya Rushwa.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Singida, Adili Elinipenda alisema, fedha zilizookolewa zimetokana na Riba Umiza katika kipindi cha Oktoba na Disemba 2020.
Matokeo ya ufuatiliaji na udhibiti wa TAKUKURU umebaini, baadhi ya wakopeshaji hawaandai Mikataba ya Ukopeshaji, Wakopeshwaji hawana Nakala za Mikataba na hata iliyopo kwa baadhi ya kampuni hizo haikidhi vigezo.
DKT. NG’WANDU “ALIJICHIMBIA KABURI DSM,TUNAFUATA MAELEKEZO”