Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul amewataka wale wote wanaojihusisha na uvuvi usiozingatia sheria na taratibu kuacha mara moja kwani Serikali haitakuwa na huruma kwa watakaokamatwa.
Gekul alitoa onyo hilo alipokuwa akiongea na wavuvi wa mkoa wa Manyara katika ziara mkoani humo, ambapo kwa mujibu wa Waziri Gekul katika operesheni iliyopita ya kupambana na uvuvi haramu ilitumika karibu bilioni 1.2 jambo ambalo alisema halivumiliki na hivyo aliwataka wavuvi kutoa ushirikiano kwa serikali ili kukomesha vitendo hivyo.
“Hatutavumilia jambo hili liendelee, Sisi kama Wizara tumesema ni lazima tupate muarobaini wa uvuvi haramu lakini na nyinyi wavuvi muwe tayari kutoa ushirikiano kwa serikali ili uvuvi haramu ukomeshwe mara moja,” Gekul