Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amezitaka Hospitali za Rufaa za Mikoa na Kanda kuanzisha miradi ya bidhaa za afya ili kuongeza kipato na kuepuka utegemezi toka Serikalini.
Waziri Gwajima amesema hayo akipotembelea kiwanda cha kuzalisha maji tiba (Infusion Unit) ya Hospitali ya Rufaa ya Tumbi iliyopo Kibaha mkoani Pwani na kuwataka kuongeza uzalishaji ili waweze kupanua soko na kuzitaka Hospitali nyingine kwenda kununua bidhaa hizo muhimu katika sekta ya afya.