Askari wa Wanyamapori toka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kituo cha Mapori ya Akiba Lukwati/Piti December 25, 2020 walipata taarifa juu ya kuwepo kwa simba katika kijiji cha Ngwala, Wilayani Songwe.
Simba huyo kwa taarifa za wenyeji alionekana kuingia kijijini hapo mida ya usiku kati ya saa tano hadi saa 10 alfajiri huku akiwa na lengo la kutafuta mbwa kijijini hapo na tayari alikwisha kamata na kula mbwa wawili.
Askari wa TAWA(Rapid Respond Team-RRT) katika kituo cha Lukwati/Piti wakaanza msako mkali wa kumtafuta simba huyo na baadaye kumuua usiku wa kuamkia Deember 27, majira ya saa 2 usiku .
Wananchi walishukuru juhudi zilizofanyika na Askari wa TAWA kwa kuwaondoa hofu na kuendelea kusherekea sikukuu ya Xmas.