Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema serikali imesitisha makongamano au mikutano ya mkesha wa mwaka mpya katika maeneo yote ya wazi leo December 31, 2020 katika mikoa yote kutokana na changamoto mbalimbali hususani za kiusalama.
Simbachawene amesema makongamano na mikutano hiyo ifanyike kwenye maeneo ya nyumba za Ibada na mwisho iwe ni saa sita na nusu usiku> “kukiwa na ulazima wa kufanya makongamano, Taasisi iombe kibali na makongamano yafanyike kuanzia saa 12 asubuhi hasi Saa 12 jioni”.