Ishara Mamboleo mtoto wa miaka sita(6) amewashangaza watu kwa uwezo mkubwa wa kupiga ala za muziki bila kukosea kwa kupitia kinanda hasa anapopata mialiko kwenye mikutano.
AyoTV na millardayo.com imezungumza na Baba mzazi Emmanuel Mamboleo kujua chimbuko la kipaji cha mtoto huyo na ni namna gani wanakiendeleza vilevile ratiba yake ya masomo.
“Tuligundua kipaji chake tangu akiwa na miaka miwili, Mama yake alikuwa akijifunza kupiga kinanda na yeye pia alikuwa anakuja anadonoadonoa kinanda pale hiyo ilitutia moyo mimi nilikuwa na mic nikaamua kutafuta mtu wa kubadilishana nae anipatie kinanda kwa njia hiyo kijana akapata kinanda cha kufanyia mazoezi” Baba mzazi wa Ishara