Ongezeko la hisa katika kampuni ya magari ya umeme ya Tesla, limepelekea leo Elon Musk kushika nafasi ya kwanza kwa utajiri duniani baada ya kufikisha umiliki wa thamani ya dollar Billion 185 sawa na Trillioni 429 za Kitanzania. Kwa sasa Elon anashika nafasi ya kwanza ambayo hapo awali ilishikiliwa na Jeff Bezo tangu mwaka 2017 ambaye kwa sasa ameshushwa nafasi ya pili kwa utajiri akiwa na Dollar Billion 184 sawa na Trilioni 426 za Kitanzania.
Utajiri wa Elon Musk unakuwa kwa kasi na mwaka 2020 aliingia katika orodha ya matajiri 50 akiwa na Dollar Billion 27 sawa na Trillion 62 za Kitanzania, na mwaka jana mwezi wa 12 alimpita Bill Gates na kushika nafasi ya pili baada ya kufikisha Dolllar Bilion 132 sawa na trilion 306 za Kitanzania.
Pia Elon bado anamiliki kiasi kikubwa cha hisa katika kampuni ya SpaceX inayosafirisha watafiti na vifaa kwenda angani; na pia anasimamia kampuni kubwa zinazosimamia teknolojia za SolarCity, Neuralink, OpenAI na Zip2 ambazo zinashika nafasi kubwa katika ubunifu kwenye teknolojia duniani.