Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limefanya ukaguzi wa kushtukiza na kupiga faini katika Kituo cha Mabasi baada ya kubaini kuondolewa na kutokuwepo kwa namba za simu za Jeshi la Polisi zinazosaidia abiria kutoa taarifa panapotokea makosa ya kiusalama barabarani.
Akizungumza wakati wa ukaguzi Afisa Oparesheni wa Mkoa wa Tabora, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Glaifton Mushi amemuagiza Mkaguzi wa magari kuhakikisha anafuatilia uwepo wa namba hizo.
“Kuna kitu mnataka kuficha ili hawa abiria wasiweze kutusaidia waandikieni faini wakalipe ndio wataweka kila mahali ili abiria waweze ku-access hii namba wanatakiwa wabandike kila mahali ili abiria waweze kuiona” SSP Mushi