Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI David Silinde amemkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Ikhanoda Kata ya Ikhanoda iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Singida Omary Selestine kwa Jeshi la Polisi na TAKUKURU baada ya kugundua matumizi mabaya ya fedha za umma katika ujenzi wa bwalo la chakula kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo.
Hatua hiyo imetokea baada ya Silinde kufanya ziara katika Shule hiyo kukagua mradi wa lipa kutokana matokeo (EP4R) ambao shule hiyo walipewa kwa ajili ya ujenzi wa bwalo lakini mpaka sasa fedha zaidi ya milion 50 zimetumika huku ujenzi ukiwa katika hatua ya msingi hali iliyopelekea Silinde kuona kuna ubadhitifu mkubwa wa fedha huku baadhi ya vifaa vikinunuliwa kwa bei ya juu sana kuliko uhalisia wa bei.
“Huwezi nunua mabati ya milioni 70 unataka kujenga nini,au unanunua tofali kwa shilingi elfu tano ni tofali aina gani,Kamanda wa Polisi na TAKUKURU mchukue huyu mwalimu na kamati nzima ya ujenzi wakaeleze wametumiaje fedha za ujenzi wa mradi huu “ Silinde