Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, amempa siku saba Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, (IGP) Simon Sirro, kushughulikia bajeti ya chakula cha mbwa wawili wanaotumika kulinda ulinzi na usalama.
Simbachawene ametoa agizo hilo Jijini DSM, wakati wa ziara ya kikazi alipotembelea maeneo ya Jiji hilo.
Amesema mbwa hao wawili kati ya saba hawana bajeti ya chakula hivyo wanatakiwa kupewa bajeti kwa sababu wanafanya kazi kubwa kuliko binadamu.
“Mbwa hawa ni askari wanaotumika sana ni nimemwagiza IGP ndani ya siku saba ahakikishe Mbwa wate saba wapo kwenye bajeti, katika mbwa saba wapo mbwa watano wenye bajeti na wawili hawapo kwenye bajeti ambapo kwa mwezi wanatumia Sh laki nane, inatakiwa wote wawepo kwenye bajeti,” Simbachawene
Aidha, Simbachawene amempa Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa zawadi ya gari kama ishara ya pongezi kwa utendaji wake ikiwa na kudhibiti uhalifu na kupungua kwa kiasi kikubwa.