Umoja wa Ulaya (EU) umepanga kutoa idhini kwa utumiaji wa ndege za abiria aina ya Boeing 737 Max kuanzia wiki ijayo, ambazo zilikuwa zimepigwa marufuku kusafiri kutokana na ajali za mara kwa mara.
Mkurugenzi wa Shirika la Usalama wa Anga la Ulaya (EASA), Patric Ky, ametoa taarifa kuhusu ndege hizo za 737 Max zinazotengezwa na kampuni ya Boeing ya Marekani, zilizokuwa zimepigwa marufuku baada ya ajali kutokea mwaka 2018 na 2019.
Ky amefahamisha kuwa ndege za Boeing 737 Max zitapewa idhini ya mwisho ya kuanza tena safari za anga barani Ulaya wiki ijayo.
Akielezea kuwa suala la jinsi ajali zilivyotokea amebainisha kuwa mabadiliko yaliyofanywa ili kuongeza usalama wa ndege yanatimiza vigezo vinavyotakiwa. Marekani na Brazil zilizindua safari za ndege za kibiashara za Boeing 737 Max mwaka jana.