Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limesema kuanzia Machi Mosi, 2021 utaratibu wa kukagua magari kutoka nje ya nchi utakuwa ukifanyika baada ya kuwasili nchini.
Kwa sasa TBS inakagua magari kutoka nje kupitia mawakala watatu mmoja Japan na mwingine Dubai ambao mikataba itakoma hivi karibuni.
Maswali yalikuwa mengi baada ya taarifa hii kutolewa January 20, 2021, AyoTV na millardayo.com imefika TBS ambapo Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora Shirika la Viwango Tanzania, Lazaro Msasalaga ametoa ufafanuzi kuhusu ukaguzi wa magari yanayotoka nje ya ya nchi utakuaje.
“Kwa utaratibu wa namna magari yatakuwa yanashushwa na kuwekwa kwenye maeneo yake maalumu kutakuwa na seti za vifaa vya ukaguzi 12, lakini kwenye hizo seti 8 zitafungwa ndani ya rore yard . Seti mbili zitafungwa kwenye yard ya magari makubwa wakati seti moja itafungwa Kitopeni kwenye magari machache ambayo yamehamishwa kutoka rore yard” Msasalaga