Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo amemuagiza Kamanda wa Polisi Mkoani humo kufanya msako wa Kijiji kwa Kijiji na kuwakamata Waganga wa kienyeji maarufu “Lambalamba”.
Pia, amewaagiza Walimu Wakuu na Wakuu wa Shule kuwakagua Wanafunzi ili kubaini iwapo wanavaa hirizi wawapo Shuleni, kama sehemu ya kukabiliana na vitendo vya kishirikina.
Amesema Waganga hao wamekuwa wakiwadanganya Wananchi, kuwadhulumu pesa zao na kuwaacha wakiendelea kuwa masikini huku akisisitiza Nchi haiwezi kuendeshwa kwa Imani za kishirikina ambazo zinarudisha nyuma juhudi za kujikwamua na umasikini.
Amemuelekeza Kamanda wa Polisi kukiweka chini ya ulinzi Kijiji kitakachoonekana kuwaficha Waganga ama kutotoa ushirikiano kwa Polisi. Asema, kuna Wazazi wanashindwa kuwahudumia Watoto wao mahitaji ya shule lakini anatumia pesa hiyo kumpatia mganga huyo ili aweze kumsafishia mji wake.