Kutoka Ipuli Mkoani Tabora, nyumbani kwa Marehemu Brig. Jen Mstaafu Emmanuel Maganga (RC Mstaafu wa Kigoma), kinachoendelea hapa muda huu ni Ibada ya kuuaga mwili na baadae utasafirishwa kuelekea Dar es salaam ajili ya kuagwa na kisha kusafirishwa tena kwenda Morogoro kwa ajili ya Mazishi.
Maganga alifariki jana saa tatu usiku katika Hospitali ya Milambo, Tabora na kwa mujibu wa RC Tabora Dr. Sengati chanzo cha kifo chake ni Presha na Kisukari ambacho kilipelekea moyo wake kufeli.