Rais mpya wa Marekani, Joe Biden amewaondolea raia wa Tanzania vikwazo vya kushiriki bahati nasibu ya viza, ikiwa ni mwaka mmoja tu baada ya kutangazwa kwa vikwazo hivyo.
Januari 30, 2020 serikali ya, Donald Trump ilitangaza kuwawekea Watanzania vikwazo vya kushiriki bahati nasibu hiyo pamoja na raia wa nchi nyingine kadhaa.
Jana Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ulitangaza kuwa marufuku hiyo imefutwa rasmi na rais mpya wa nchi hiyo, Joe Biden aliyeingia madarakani juzi.
“Mojawapo kati ya hatua zake za mwanzo kabisa akiwa Rais, Biden ameondoa kikwazo kilichowekwa kwa Watanzania kuomba Viza ya Bahati Nasibu (Diversity VISA – DV),” ubalozi huo umeandika kupitia ukurasa wake wa Twitter.