Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile ameiarifu Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuwa Tsh. Trilioni 18 zinapita kwenye mitandao kwa mwezi, wakati wa kikao chake na kamati hiyo kilichohudhuriwa na wajumbe wa Menejimenti ya Wizara hiyo na wakuu wa taasisi zake, Dodoma.
Dkt. Ndugulile amewaeleza wajumbe wa Kamati hiyo kuwa miamala Milioni 300 inafanyika kwa mwezi mtandaoni na Serikali inapata Tsh. Bilioni 80 kwa mwezi za tozo kutokana na fedha zinazopita mtandaoni na mzunguko huo wa fedha mtandaoni kwa mwezi, miamala inayofanyika na tozo ambazo Serikali inapata ni kutokana na kuwepo kwa matumizi ya TEHAMA
Amesema Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ni njia kuu ya uchumi na inawezesha upatikanaji wa huduma za mawasiliano yenye kasi, kufanikisha utendaji kazi wa mifumo ya TEHAMA na huduma za fedha mtandaoni ambapo Wizara imejipanga kuandaa ramani ya njia ya miundombinu huo ili kufanikisha mwingiliano wa ujenzi na upanuzi wake pale inapokutana na njia za miundombinu mingine kama vile ya barabara, maji, umeme na reli.
MWANAFUNZI ALIEONGOZA KIDATO CHA 4 NCHI NZIMA APOKELEWA KWA ULINZI AIRPORT, MABODYGUARD WATAPAKAA