Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi amelipongeza Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa kuendelea na kazi kubwa ya kuimarisha amani hasa kipindi cha uchaguzi na kuilinda mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais Mwinyi ameyasema hayo leo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Tanzania (CDF) Jenerali Venance Mabeyo, aliyefika Ikulu Jijini Zanzibar kwa ajili ya kumpongeza.
“Zanzibar iko salama na kwa vile Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) lipo imara hatua hiyo imepelekea kuimarika zaidi.” Mwinyi
Nae Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Tanzania (CDF) Jenerali Mabeyo kwa upande wake alipongeza hatua na busara kubwa zilizotumika katika kuleta maridhiano hali ambayo itazidisha maelewano sanjari na kudumisha amani na umoja nchini.
LIVE: HAJI MANARA NA KOCHA WA AL-HILAL MBELE YA WAANDISHI WA HABARI