Polisi Kigoma wanawashikilia Watu watatu kwa tuhuma za wizi wa nyaya za umeme mali ya TANESCO zenye thamani ya Tsh. Milioni 24 wanazotuhumiwa kuziiba kwenye mradi wa kusambaza umeme vijijini REA Kasulu.
Taarifa kutoka kwa Raia wema zilikuwa chanzo cha kubaini njama za Wahalifu hao ambao waliiba rola nne za nyaya hizo wakiwa na gari mbili aina ya Fuso T 652 AQW na nyingine T 909 DBW ambapo Fuso moja imetambulika kuwa inamilikiwa na Mkandarasi anaejenga mradi wa umeme Vijijini (REA) Katavi.
“Watuhumiwa hao baada ya kukamatwa walifanyiwa mahojiano na kukiri kuiba nyaya hizo na kwamba walikua wanakwenda kuziuza mwanza kwenye viwanda vinavyoyeyusha kwaajili ya kutengeneza masufuria” – RPC Kigoma